Wednesday, January 30, 2013

Harusini na Sinta

Mdau wa BLUE PALACE fuatilia kipindi hiki cha Harusini na Sinta ili upate kuona huduma zinazotolewa ndani ya BLUE PALACE plzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz Usikose....

HARUSINI NA SINTA NDANI YA BLUE PALACE

Hapa Sinta akiwa ndani ya Saloon  ya Kisasa inayofahamika kama Blue Palace iliyoko maeneo ya Sinza mapambano kwaajili ya kuaandaa kipindicha Television ya DTV kinacholuka hewani kila siku ya Juma nne saa 3:00 usiku
 
Mmmmm....!!!!!! Raha saaaaannnaaaaa mmmmmmmmmmm.......!!!! Hapa Sinta akifanyiwa Message  wakati wa aandalizi ya Kipindi Huku akipata raha na burudani ya Huduma hiyo ........

Monday, January 14, 2013

Tunza Mikono na Miguu yako.



Miguu kama sehemu nyingine za mwili isipoangaliwa vizuri huweza leta madhara kiafya. Ni vizuri miguu ikatunzwa vizuri kuanzia viatu vinavyovaliwa hadi jinsi ya kuisafisha. Kuna aina mbalimbali za viatu mfano viatu vya kufunika vifupi, viatu virefu vya wazi, viatu vifupi vya wazi na viati virefu vya kufunika. Viatu vyote hivi huwa vinakuwa na muundo tofauti kadiri mvaaji anavyopendelea.
Ni vizuri kuepuka kuvaa viatu virefu sana mara kwa mara na hasa kama unatembea navyo kwa muda mrefu maana husababisha matatizo kwenye misuli ya miguu kama vikivaliwa mara kwa mara na kwa muda mrefu. Pia ni vyema kutovaa viatu vya kufunika na vyenye joto sana kwa muda mrefu hasa sehemu zenye joto kali maana huweza leta matatizo kwenye miguu. Vile vile si vyema kuvaa viatu vya wazi nje kama sehemu inabaridi kali na barafu.
Ili miguu yako iweze kuwa na uzuri wa asili siku zote basi ni vizuri angalau mara moja kwa wiki uwe na siku maalumu ya kusafisha miguu yako (sio kwamba siku nyingine husafishi, la hasha hapa naongelea usafi maalum). Andaa maji ya uvuguvugu na uweke nyenye beseni pamoja na sabuni ya maji ambayo ina dawa (medicated).  Kisha kata kucha zako vizuri na kama utapendelea basi uisugue miguu yako kwa kutumia mafuta maalumu ya kusugulia kuanzia kwenye magoti hadi vidoleni (scrub).Kisha loweka kwenye maji kwa muda wa dakika tano.
Baada ya hapo nawa vizuri na kusugua unyayo kwa kifaa maalumu au jiwe laini kisha suuza miguu yako na maji safi. Baada ya hapo kausha vizuri na upake mafuta mazuri kwa ajili ya kulinda ngozi ya miguu. Hakikisha uchafu wote umetoka na hasa kwenye kucha na vidole.
Tunza miguu yako vizuri maana ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Mungu akubariki sana.

Sunday, January 13, 2013

Je, Unafahamu Kuhusu Pochi?



Pochi ni sehemu muhimu sana katika maisha ya mwanamke. Pochi zipo za aina, rangi, ukubwa na matumizi mbali mbali. Ni nadra sana kukutana na binti au mama anayetembea bila pochi, na kwa wengine maisha yao yote wanatembea nayo kwenye pochi.
Kuna vitu muhimu ambavyo ni lazima kila mwanamke akumbuke kutembea navyo kwenye pochi, na kuna vingine ni vyema kuwa navyo lakini sio lazima.
Muhimu
1. Pini
2. Sindano na uzi
3. Vifungo
4. Dawa yoyote ambayo unaitumia na kuihitaji
5. Kitambulisho
6. Pedi
7. Kalamu na notebook
Ukipenda
1. Perfume
2. Lip shiner / lip stick
3. Poda
4. Kitana
5. Khanga / mtandio
6. Kadi ya benki
7. Sandals kama unavaa viatu virefu

Thursday, January 10, 2013

Five Kali











Wow!


Huyu ni moja ya wadau na mteja wa BLUE PALACE akiwa ndani ya Saloon ya Blue Palace iliyoko Sinza

Namna bora ya kutunza miguu

Sasa tuzungumzie juu ya utunzaji wa miguu. Miguu ni sehemu inayoangaliwa sana hasa kwa wanawake, kwani unapoamua kuvaa nguo fupi na huku miguu yako haiko katika hali ya kuvutia sina shaka utaanza kujishuku hata kabla ya kutoka nje.
Miguu ni sehemu ambayo inatakiwa kutunzwa kwa kipekee kama ilivyo sehemu nyingine kama uso. Wengi tumekuwa tukipendezesha nyuso zetu na kusahau kbisa habari za miguu.

Haijlishi miguu yako ni miembamba au minene iwapo utaitunza vizuri sina shaka kuwa utavutia kwa nguo yoyote utakayoivaa.
Kuna njia nyingi za kutunza miguu na unaweza kutunza miguu yako hata kama huna fedha za kununulia vikorokoro vinavyotakiwa.
Unaweza kuchukua beseni na kuweka maji ya uvuguvugu yenye povu la sabuni maalum ya kuoshea miguu kisha loweka miguu na iache kwenye maji kwa muda wa robo saa hivi.
Chukua aina ya scrub uliyoichagua kwa ajili ya miguu yako paa na ikikauka anza kusugua miguu yako na hadi kwenye vidole na unyayo.
Kisha jisafishe kwa maji ya uvuguvugu.
Baadhi ya vitu unavyoweza kutumia ili ku kutengeneza miguu yako ni pamoja na foot file, Therapysa virgin vie salt scrub, Pedicure iliyotengenezwa kwa OPI Refresh Cooling ffot Gel, Innoxa cool na Calm liquid talc na Feet first reviving Foot Soak.
Bidhaa hizi unaweza kuzipata kwenye duka kubwa la vipodozi na pia utpata maelezo jisi ya kutumia
Pia unaweza kutembelea baadhi ya saluni ambazo zinatoa huduma hiyo jitahidi hata mara moja kwa mwezi kuhakikisha miguu yako inapata huduma nzuri ili iwe ya kuvutia.
Kwa wale ambao miguu yao ni makovu au madoadoa wajaribu kutumia scrub na kama hawatafanikiwa kuondoa tatizo hilo basi wanashauriwa ktumia cream na sabuni zenye mchanganyiko wa ukwaju kwani

zinasaidia sana kuondoa madoa.
Pia unaweza kuchukua mkwaju ukaloweka kwenye maji ukishalainika changanya mchanganyiko huko na asali kasha paka.
Husaidia kuondoa madao na hata kwa wale wenye ngozi za mafuta na chunusi sugu mafuta yatakauka na chunusi hazitatoka tena.