Thursday, January 10, 2013

Namna bora ya kutunza miguu

Sasa tuzungumzie juu ya utunzaji wa miguu. Miguu ni sehemu inayoangaliwa sana hasa kwa wanawake, kwani unapoamua kuvaa nguo fupi na huku miguu yako haiko katika hali ya kuvutia sina shaka utaanza kujishuku hata kabla ya kutoka nje.
Miguu ni sehemu ambayo inatakiwa kutunzwa kwa kipekee kama ilivyo sehemu nyingine kama uso. Wengi tumekuwa tukipendezesha nyuso zetu na kusahau kbisa habari za miguu.

Haijlishi miguu yako ni miembamba au minene iwapo utaitunza vizuri sina shaka kuwa utavutia kwa nguo yoyote utakayoivaa.
Kuna njia nyingi za kutunza miguu na unaweza kutunza miguu yako hata kama huna fedha za kununulia vikorokoro vinavyotakiwa.
Unaweza kuchukua beseni na kuweka maji ya uvuguvugu yenye povu la sabuni maalum ya kuoshea miguu kisha loweka miguu na iache kwenye maji kwa muda wa robo saa hivi.
Chukua aina ya scrub uliyoichagua kwa ajili ya miguu yako paa na ikikauka anza kusugua miguu yako na hadi kwenye vidole na unyayo.
Kisha jisafishe kwa maji ya uvuguvugu.
Baadhi ya vitu unavyoweza kutumia ili ku kutengeneza miguu yako ni pamoja na foot file, Therapysa virgin vie salt scrub, Pedicure iliyotengenezwa kwa OPI Refresh Cooling ffot Gel, Innoxa cool na Calm liquid talc na Feet first reviving Foot Soak.
Bidhaa hizi unaweza kuzipata kwenye duka kubwa la vipodozi na pia utpata maelezo jisi ya kutumia
Pia unaweza kutembelea baadhi ya saluni ambazo zinatoa huduma hiyo jitahidi hata mara moja kwa mwezi kuhakikisha miguu yako inapata huduma nzuri ili iwe ya kuvutia.
Kwa wale ambao miguu yao ni makovu au madoadoa wajaribu kutumia scrub na kama hawatafanikiwa kuondoa tatizo hilo basi wanashauriwa ktumia cream na sabuni zenye mchanganyiko wa ukwaju kwani

zinasaidia sana kuondoa madoa.
Pia unaweza kuchukua mkwaju ukaloweka kwenye maji ukishalainika changanya mchanganyiko huko na asali kasha paka.
Husaidia kuondoa madao na hata kwa wale wenye ngozi za mafuta na chunusi sugu mafuta yatakauka na chunusi hazitatoka tena.

No comments:

Post a Comment